Mh. W. LUKUVI ALIFUNGUA JENGO LA BALAZA LA ARDHI WILAYA KISHA ALIPATA FURSA YA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA ENEO LA VIWANJA VYA CHINI YA MTI MJINI KIBAYA.
PICHA ZA MATUKIO HAYA NI HIZI ZIFUATAZO:-
 |
Hili ni jengo la Baraza la Ardhi Wilaya lilipo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara. Jengo hili limezinduliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Wiliam Lukuvi leo tarehe 07.06.2016.
|
 |
Mh. Lukuvi akiwahutubia wananchi katika Viwanja vya chini ya mti katikati ya Mji wa Kibaya Wilayani Kiteto
Hii ni meza kuu, kwa majina kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kiteto Mh. Lailumbe, anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto
Mh. Col. S. Nzoka, kisha Waziri Mh. Wiliam Lukuvi,
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera na wamwisho ni
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. E. Papian
Mh. Waziri akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera akisalimiana na Mzee maarufu wa Wilaya ya Kiteto.
Upande wa kulia wanaoonekana ni Wataalamu mbalimbali
waliohudhuria katika mkutano huo
Wananchi wa Wilaya ya Kiteto wakimsikiliza Mh. Lukuvi akiwahutubia.
Viongozi wa Serikali kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Mkoa wa Manyara kwa ujumla wao wakiwa wamejumuika na wananchi katika viwanja hivyo wakimsikiliza Mh. Lukuvi akiwahutubia.
Vyombo vya ulinzi na usalama havikuwa mbali katika kuhakikisha uwepo wa usalama wa raia katika mkutano huu, kama wanavyoonekana katika gari hapo juu.
Kisha Wananchi mbalimbali walipata fursa ya kuuliza maswali kwa Serikali kama inavyoonekana picha za hapo chini.
|

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Bosco O. Ndunguru (wa upande wa kushoto) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vilivyohusu Ardhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Bosco O. Ndunguru (aliyesimama mbele katikati) akiendelea na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vilivyohusu Ardhi.
Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Kiteto Bw. S. Kasturi (aliyesimama wa kwanza kushoto ) akitoa ufafanuzi katika vipengele vilivyohusu Ujenzi.
Kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya ya Kiteto Bw. Guricha akitoa ufafanuzi katika vipengele vilivyohusu Ardhi.
No comments:
Post a Comment