Friday, 22 July 2016

HALMASHAURI YA WILAYA YA KITETO YAMKARIBISHA RASMI MKURUGENZI MTENDAJI (W) MPYA Bw.TAMIM KAMBONA NA KUMUAGA MKURUGENZI MTENDAJI (W) Bw. BOSCO O. NDUNGURU AMBAYE ANAHAMIA MANISPAA YA TABORA MKOA WA TABORA LEO TAREHE 22.07.2016

HOIHOI NDEREMO NA VIFIJO VILITAWALA KATIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE HAPA MJINI KIBAYA BAADA YA KUFANYA HAFLA FUPI YA KUMKARIBISHA Bw. TAMIMU KAMBONA (MKURUGENZI MPYA) NA KUMUAGA Bw. BOSCO O. NDUNGURU MKURUGENZI ANAYEHAMIA MANISPAA YA TABORA MJINI MKOA WA TABORA.

KATIKA HAFLA HII MGENI RASMI ALIKUWA NI MKUU WA WILAYA YA KITETO AMBAYE ALIWAKILISHWA NA Bw. MASSINDE. MGENI RASMI ALISIFU MNO  KWA KUTAMKA KWAMBA Bw. NDUNGURU NI KIONGOZI MWENYE UWEZO MKUBWA SANA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO NZITO ZILIZOKUWA ZINAIKABILI HALMASHAURI KAMA VILE KUHAKIKISHA AMANI INAPATIKANA, KUWA NA HATI SAFI NA KUONGEZA UFANISI WA UKUSANYAJI WA MAPATO.

HAFLA HII ILIFANA SANA KWA KUAMBATANA NA BURUDANI, SHAMRA SHAMRA NA MATUKIO MENGINE MENGI, FUATANA NASI KATIKA BLOGU HII UJUE HALI ILIKUWAJE:-

Mgeni Rasmi Bw. Massinde toka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali, Mashirika ya Umma na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika Hafla hiyo.




Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkaribishwa Bw. T. Kambona, wapili ni Mkurugenzi  anayeagwa  Bw. Bosco O. Ndunguru, watatu ni Mgeni Rasmi Bw. Massinde aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, na wa mwisho ni Makamu Mwenywkiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mh. Masumbuko aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri  (W).











Picha zinazoonekana hapo juu ni watumishi mbalimbali wakiwa wanapata vinywaji moto na baridi taratibu kabisa katika Hafla hiyo.



Afisa Maendeleo ya Jamii toka Halmashauri Bi. Janeth akiwa katika zoezi la ufunguaji wa Champaign kama ishara ya upendo.



Wageni wetu wakiwa tayari kwa hekaheka (Cheers) na wote waliohudhuria katika Hafla hiyo.






















Kisha burudani motomoto iliendelea sanjari na vinywani kama unavyojionea mwenyewe mpenzi msomaji. 









Ndipo ulifika wakati wa kupokea zawadi toka Halmashauri (W), Mashirika mbalimbali  ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali pamoja na watu binafsi.

Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkaribishwa Bw. T. Kambona, wapili ni Mkurugenzi  anayeagwa  Bw. Bosco O. Ndunguru, watatu ni Mgeni Rasmi Bw. Massinde aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, na wa mwisho ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mh. Masumbuko aliyemuwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri  (W).




Hawa ni wafanyakazi toka Benki ya CRDB tawi la Kibaya Mjini wakitoa zawadi.




Hawa ni wafanyakazi toka Chama cha Waaalimu tawi la Kiteto  wakitoa zawadi.






Hawa ni wafanyakazi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) huyu mwenye nguo nyeupe kulia ni Katibu Muhtasi Bibi Partricia Kabadi.


Kulia wa kike ni Bibi Hawa


Kulia ni Dreva wa Mkurugenzi Bw. Masoud



Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto wakimvisha Shuka la  tamaduni za wakazi wa Kiteto Mkurugenzi (anayeagwa) Bw. Ndunguru ikiwa ni ishara ya kutambua ushirikiano  wa dhati aliouonyesha katika jamii ya Kiteto akiwa kiongozi. 


Pia Bw.Ndunguru alipewa kirungu cha jadi ikiwa ni ishara ya ulinzi popote atakapokwenda.



Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto wakimvisha Shuka la  tamaduni za wakazi wa Kiteto Mkurugenzi anayekaribishwa  Bw. Kambona ikiwa ni ishara ya kumpokea na kumpa ushirikiano  wa dhati katika kazi. 









Kisha kamati tendaji ya Hafla hii kwa  niaba ya watumishi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ilitoa zawadi.



Mgeni Rasmi akitoa nasaha zake kwa wageni waalikwa.



Hapo chini, Mgeni Rasmi akichukua chakula.


Makamu Mwenyekiti Mh. Masumbuko  akichukua chakula wa kwanza mbele.



Wapili kutoka kulia Bw. Ndunguru  naye akichukua chakula.



Wakwanza kutoka kulia Bw. Kambona (Mkurugenzi Mtendaji W)  akichukua chakula.



Kisha wengine walifata baada ya meza kuu kuchukua chakula.







Ndipo ilifika wakati wa burudani kali iliyowasisimua wote waliohudhuria kutovumilia kukaa bali kulisakata rhumba kama unavyoona mpenzi msomaji.











No comments:

Post a Comment